UNAWEZA kusema kuwa mwisho wa mwaka 2016 huenda na matukio ya vioja. Kimetokea kituko cha aina yake katika Mitaa ya Isanga Jijini Mbeya Mkoa wa Mbeya mara baada ya bwanaharusi kuingia mitini masaa machache kabla ya kufunga ndoa. Tukio hilo la aina yake limeibua maswali mengi kwa ndugu jamaa na marafiki ambao walikuwa tayari kwa maandalizi ya kuhudhuria harusi hiyo kuanzia kanisani hadi ukumbini.
Imeelezwa kuwa mipango yote ya harusi ilifanyika kwa pande zote mbili kushiriki kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa hadi hatua ya mwisho ya kuingia kanisani ambapo kama kawaida ndugu jamaa wote walihudhuria kanisani kwa lengo la kushuhudia tukio hilo. Tukio rasmi lilianza majira ya saa 7 mchana katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Isanga jijini Mbeya Desemba 16 ambapo kama kawaida Bibi harusi akiongozana na wapambe wake akifuata na msafara wa magari zaidi ya
manne akitokea Saloon na kuingia kanisani hapo.
manne akitokea Saloon na kuingia kanisani hapo.
Baada ya bibi harusi kuingia kanisani tayari kwa kufunga ndoa hiyo taarifa zilianza kuenea kuwa bwanaharusi hayupo kanisani hapo na hajulikani mahali alipo. Kadri muda ulivyozidi kwenda bila bwana harusi kufika kanisani hapo baadhi ya Ndugu, jamaa na watu waliohudhuria harusi hiyo walianza kuhoji ambapo kwa muda huo yalipita zaidi ya masaa 4 bila chochote kuendelea kanisani hapo.
Kadi ya mualiko kwa ajiliya sherehe |
Bibi harusi Given Mgaya Mkazi wa Isanga jijini Mbeya |