Bunge Sports Club yaibuka Kidedea Mechi za Kirafiki na NMB

Spika wa Bunge Job Ndugai akimkabidhi kikombe Naodha wa timu ya Bunge Sports Club ambaye ni Mbunge wa Mbiga, Sixtus Mapunda baada ya timu hiyo kuifunga NMB Magori 2-0 wakati wa mchezo wa kirafi uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

 

Wachezaji wa Bunge Sports Club na NMB mpira wa pete wakiwania mpira wakati wa mchezo wa kirafi uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

 

Abdulmajid Nsekela- Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na wa kati NMB akisalimiana na mchezaji wa Bunge Sports Club mpira wa Pete ambaye ni Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kabla ya mchezo wa kirafiki wa Pete kati ya Bunge na NMB.

 

Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Straton Chilongala akimkabidhi nahodha wa mpira wa Pete wa Bunge Sports Club ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Esther Matiko.

 

Abdulmajid Nsekela akikabidhi kikombe cha mpira wa Kikapu kwa washindi Bunge Sports Club.

TIMU ya Bunge Sports Club inayojumuisha timu ya mpira wa miguu, mpira wa pete na kikapu imeibuka washindi na kunyakua vikombe vitatu katika bonanza lililozikutanisha timu ya Bunge na timu ya Benki za NMB.

Timu ya kwanza ya Bunge kushinda kikombe ilikuwa timu ya mpira wa pete ambaye iliifunga timu ya pete ya NMB magoli 19 kwa 2, ikifuatiwa na timu ya mpira wa kikapu kwa wanaume ambayo iliwafunga wapinzani wao timu ya mpira wa kikapu ya NMB kwa jumla ya vikapu 37 kwa 28.

Kikombe cha tatu kwa timu ya Bunge kilipatikana kwa timu ya mpira wa miguu ambayo iliwafunga NMB goli 2-0 na hivyo kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote ambao timu hizo zimekutana.

Timu ya Bunge Sports Club na NMB Sports Club zimekuwa zikikutana zikicheza michezo mbalimbali ikiwa na lengo ya kuboresha uhusiano baina ya Bunge na NMB ambapo kwa mwaka huu bonanza hilo limefanyika katika uwanja wa Jamhuri uliopo makao makuu ya nchi, Dodoma.

 

Spika wa Bunge, Job Ndugai akisalimiana na wachezaji wa mpira wa kikapu wa Timu ya NMB ya mchezo huo muda mfupi kabla ya mpambano wa mchezo wa mpira wa kikapu kati ya Timu ya Bunge na NMB. Katika mpambano huo Bunge ilishinda kwa vikapu 37 kwa 28 vya NMB. Wakati wa mchezo wa kirafi uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.