Bunge lataka EWURA CCC iongezewe bajeti

Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA,Haruna Masebu

Na Magreth Kinabo–MAELEZO

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya umma (PAC), imeagiza sheria inayoruhusu Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (EWURA) kulipa mishahara ya watumishi wa Baraza Ushauri na Watumaji la Nishati la EWURA (EWURA CCC) ibadilishwe ili baraza hilo liweze kufanya kazi ipasavyo.

Hayo yalisemwa leo na Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam kuhusu shughuli zilizofanywa na Kamati yake, ambapo amesema baraza hilo hesabu zake zinakwenda vizuri.

“Baraza hili hesabu zake ni nzuri, lakini halifanyi kazi ipasavyo kwa kuwa halimtendei kazi ipasavyo liko pamoja na EWURA tumeagiza sheria ibadilishwe ili liweze kufanya kazi kwa kuzingatia pande zote,” alisema Filikunjombe.

Makamu Mwenyekiti huyo alishauri kuwa ni vyema mishahara hiyo ilipwe na wizara husika ili baraza hilo lifanye kazi bila kuegemea upande mmoja.

Akizungumzia kuhusu upandaji wa umeme kwa asilimia 40 alihojia upanda kwa sababu zipi je mlaji wa chini wamemsikiliza wanasemaje, hivyo alisema haitakuwa sahihi ikiwa hakusikilizwa.

Aliongeza kuwa baraza hilo pia linatakiwa kuacha kulipa malipo ya kila baada ya miaka mitano mtumishi anapostaafu badala yake yawe katika mfumo ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ikiwemo kuwaingiza watumishi wake katika Mfuko wa Bima ya Afya ili kuepuka utumiaji wa risiti za malipo ya matibabu.

Alitaka baraza hilo kutumia fedha kulingana na bajeti yake. Wakati huohuo Filikunjombe alisema kamati hiyo imemfukuza mwakilishi wa Shirika Hodhi la Mali za umma (CHC) kwa kuwa ni Mtendaji wa chini hawawezi kuzungumza naye hivyo wanamtaka Ofisa Mtendaji Mkuu. Alisema mwakilishi aliyetumwa ni Ofisa Uhusiano ambayo ameitumwa na Kaimu Mkurugenzi.