Bulembo Awataka Viongozi wa CCM Rombo Kushirikiana

WENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM), Abdalah Bulembo


Yohane Gervas, Rombo

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM), Abdalah Bulembo amewataka viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuondoa chuki na makundi ndani ya chama hicho.

Bulembo alitoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake wilayani Rombo ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, na kuangalia uhai wa chama hicho katika Wilaya ya Rombo.

Aidha Bulembo amewataka madiwani wa chama hicho kusimamia vyema miradi ya maendeleo inayoibuliwa na CCM ili kujenga imani kwa wananchi. Aliongeza kuwa endapo madiwani watashirikiana na viongozi wa vijiji na wananchi kusimamia na kutekeleza kwa wakati miradi hiyo itawafanya wananchi wazidi kuwa na imani na Chama Cha Mapinduzi.

Hata hivyo aliwataka wazazi wa jumuiya hiyo kutowaonea aibu watu wanaowapa mimba wanafunzi, na badala yake kuhakikisha wanawafikisha katika vyombo vya dola ili wachukuliwe hatua za kisheria.