BREAKING NEWZZZ, Madereva Ubungo wagoma

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam

Taarifa zilizotufikia asubuhi hii ni kwamba madereva wa mabasi ya kutoka Dar es Salaam kuelekea mikoani wamegoma kufanya safari zao na hadi sasa hakuna basi lolote lililoondoka kutoka kituo kikuu cha mabasi hayo cha Ubungo.

Kwa mujibu wa abiria mmoja ambaye ni msafiri ameiarifa dev.kisakuzi.com kuwa miongoni mwa mambo ambayo madereva hao wanadai ni vitendo vinavyofanywa na askari wa usalama barabarani vya kuyakamata hovyo mabasi yao ikiwa ni pamoja na kuomba rushwa.

Taarifa zinaeleza kuwa madereva hao wamegoma kufanya safari hizo hadi pale ufumbuzi wa malalamiko yao utakapo fanyiwa kazi na wao kufanya safari zao bila vikwazo vyovyote. Mwandishi wa dev.kisakuzi.com tayari amefika eneo la tukio na taarifa zaidi zitatolewa muda si mrefu.