Breaking Newzz; Wananchi Mbeya Wazuia Malori Ya Mafuta Kupita, Wafunga Barabara

TAARIFA ambazo zimetufikia muda huu ni kwamba wananchi wenye hasira mkoani Mbeya wamefunga barabara eneo la Kwa Mama John na kuzuia malori ya mafuta yanayosafarisha mafuta kwenda nchi mbalimbali kupitia mkoa hiyo kwa kile kukasirishwa na wao kuwa na uhaba mkubwa wa mafuta, ilhali nishati hiyo inapitishwa kwenda nchi jirani.

Taarifa zaidi zinasema wananchi hao wametishia kuchoma moto lori lolote litakalo vuka eneo hilo. Mtandao huu unafuatilia tukio hilo kwa karibu na tutaendelea kuwaletea taariza zaidi za tukio hilo.