ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefanikiwa kutetea nafasi yake tena ya kukiongoza chama hicho baada ya kushinda katika uchaguzi wa chama hicho uliyofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata kutoka katika eneo la uchaguzi, Freeman Mbowe ametwaa kiti hicho tena baada ya kushinda kwa kura 775 kati ya 811 zilizopigwa na kumbwaga vibaya mpinzani wake. Katika nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Prof. Abdallah Safari amefanikiwa kuibuka mshindi huku Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar akiibuka mshindi Said Issa Mohamed.
Uchaguzi huo wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA pia unatarajiwa kutoa maazimio mbalimbali ya kitaifa kuhusiana na mustakali wa Chama hicho hususan kuhusu suala la Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwakani. Habari zaidi juu ya uchaguzi huo endelea kufuatilia hapahapa dev.kisakuzi.com.
Updates: Habari za kina zinasema kwenye uchaguzi huo, Mbowe alipata kura 789 sawa na asilimia 97.3 na kumshinda mpinzani wake ambaye hakuwa na nguvu kubwa, Gambaranyera Mongateo aliyeambulia kura 20 sawa na asilimia 2.5
Hiki ni kipindi cha tatu kwa Mbowe kupewa ridhaa ya kuongoza chama hicho kikuu cha upinzani nchini. Katika kinyang’anyiro hicho, wagombea walikuwa watano, wawili walienguliwa na mmoja, Kansa Mbarouk alijitoa.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Bara), Profesa Abdallah Safari aliibuka mshindi kwa kupata kura 775 sawa na asilimia 95 baada ya kubaki mgombea pekee kwani mpinzani wake, Fred Mpendazoe alijitoa. Kura za hapana zilikuwa 34 sawa na asilimia 2.3. Jumla ya wapiga kura walikuwa 811. Kwa Zanzibar, Said Issa Mohamed alitetea nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti kwa kupata kura 645 sawa na asilimia 79.6 dhidi ya Hamad Yusuf aliyepata kura 164 sawa na asilimia 20.2. Waliopiga kura ni 810.