BREAKING NEWS:Mwanamuziki Issa Kijoti wa 5 Star, wenzake watano wafariki kwenye ajali Morogoro

Baadhi ya wanamuziki wa Kundi la 5 Star wakiwa pichani.

TAARIFA zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kuwa, wanamuziki wa kundi la 5 star wamepata ajali mbaya eneo la Mikumi Morogoro na watu watano akiwemo muimbaji maarufu wa kundi hilo Issa Kijoti wamefariki dunia.

Taarifa zinasema ajali hiyo imetokea baada ya gari lililokuwa limewabeba wanamuziki wa kundi la taarabu la 5 Star, kugongana uso kwa uso na roli la mbao, wakati wakitokea mikoani kuja Dar es Salaam.

Inasemekana waliotambuliwa kufariki dunia mpaka sasa ni pamoja na Issa Kijoti, Hamisa Omary, Husna Mapande, omary Hashim, Nasor na Shaby Juma. Taarifa zaidi kutoka eneo la tukio zinasema tayari miili ya marehemu hao imeondolewa eneo la ajali na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Morogoro.

Mdau mmoja wa masuala ya muziki amethibitisha kupatwa na ajali kwa wanamuziki hao, kwani amedai simu zao zinapigwa na kuita bila majibu kati ya kundi lililokuwa likisafiri katika gari hilo.

Inadaiwa jumla ya watu sita (6) wamefariki dunia katika ajali hiyo. Taarifa zaidi zitatolewa na The Habari kadri zitakavyotufikia, endelea kufuatilia.