Mbunge wa Chadema anayeliwakilisha jimbo la Ubungo John Mnyika aondolewa katika kikao cha Bunge kilichokuwa kikijadilia bajeti ya mwaka 2012/2013.
Mbuge huyo alitolewa baada ya kutumia maneno makali dhidi ya rais na ambayo yalikiuka kifungu N0. 64 cha Bunge ambacho alikataa kufuta na kupelekea kuondolewa katika kikao hicho muhimu na kupelekea kukosa kikao cha leo katika kuchangia bajeti.
Naibu spika alikemea vikali tabia za wabunge kutumia matusi maneno yanayoudhi ama kukikuka maadili ya bunge hivyo kuwataka wabunge wote kutumia nafasi zao kuwawakilisha vilivyo wananchi wao kwani wao ndio waliowapa dhamana ya kuwepo mahala hapo.