Breaking News, Chadema wapigwa mabomu Dar

Na Joachim Mushi, Thehabari, Dar es Salaam

TAIFA  ambazo mtandao wa dev.kisakuzi.com umezipata muda huu ni kwamba Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Dar es Salaam wamelazimika kuwatawanya vijana wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wanaandamana kuelekea kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, anakoshikiliwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe.

 Taarifa zinadai kuwa vijana hao walikuwa wakiandamana kwenda kituoni hapo kasha baadaye kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kama ishara ya kupinga kitendo cha kukamatwa kwa kiongozi wao (Mbowe).

 Polisi wamewatawanya vijana hao huku ikiwa ni muda mfupi tangu chama hicho kitoe kauli kali iliyotolewa na Dk. Slaa kuwa wapo tayari kuwaruhusu wafuasi wao kuandamana nchi nzima kupinga kitendo cha kukamatwa kwa viongozi wao.

 Tangu jana polisi jijini Dar es Salaam wamekuwa katika hali ya tahadhari hasa sehemu ya kituo kikuu ambacho Mbowe anashikiliwa. FFU wakiwa na magari ya maji ya kuwasha wakijihadhari na chochote kitakacho tokea kufuatia kwa hatua yao hiyo.

Wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wamekusanyia pembeni eneo la kituo hicho kikuu cha polisi anachoshikiliwa.