Brazil Wapuuza Uvumi wa Maandamano Michuano ya Olimpiki

olimp

Maafisa nchini Brazil wamepuuza vitisho vya kuzuka maandamano makubwa wakati wa michezo ya Olimpiki, licha ya mgogoro wa uchmi na kisiasa na sakata linalochipuka la ufisadi katika kampuni ya serikali ya mafuta, Petrobas

Waziri wa UIinzi wa Brazil Aldo Rebelo anasema anatarajia kuwa maafisa wa usalama 85,000, wakiwemo wanajeshi 38,000 watatosha kuhakikisha usalama wakati wa mashindano hayo ya Rio de Janeiro kuanzia Agosti tano hadi 21.

Baadhi ya makundi ya wakaazi wa Rio de Janeiro wameahidi kuandamana tena wakati wa michezo hiyo, hasa yale yanayowawakilisha watu walioachwa bila makaazi kutokana na miradi ya ujenzi kwa ajili ya Olimpiki.