Brazil, Ujerumani Zaingia Nusu Fainali Kombe la Dunia

David Luiz wa Brazil akishangilia baada ya kufunga bao la pili la timu yake.

David Luiz wa Brazil akishangilia baada ya kufunga bao la pili la timu yake.

Mchezaji wa Brazil, Neymar da Silva akipelekwa hospitali baada ya kuchezewa vibaya.

Mchezaji wa Brazil, Neymar da Silva akipelekwa hospitali baada ya kuchezewa vibaya.

TIMU ya Taifa ya Brazil imefanikiwa kuingia nusu fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuibugiza Timu ya Taifa ya Colombia mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika katika uwanja wa Estadio Castelao, nchini Brazil.

Mabao ya Brazili yalifungwa na Thiago Silva dakika ya 7, kabla ya David Luiz kumalizia tena dakika ya 68 kwa kuifungia timu yake. Colombia waliambulia goli pekee la penati lililofungwa na mchezaji, James Rodríguez katika dakika ya 80 ya mchezo huo uliokuwa na upinzani mkali.

Licha ya ushindi huo Brazil imejikuta katika furaha na machungu baada ya mshambuliaji wao nyota, Neymar da Silva kukimbizwa hospitalini ghafla baada ya kuchezewa vibaya na mmoja wa wachezaji wa Colombia. Kwa ushindi huo Brazil watapambana na Ujerumani.

Katika mchezo wa robo fainali ya kwanza kati ya Ufaransa na Ujerumani, Wafaransa walijikuta wakiangukia pua baada ya kubugizwa bao moja kwa mtungi na Wajerumani. Mfungaji wa goli pekee lililoipa Ujerumani ushindi ni mchezaji, Mats Hummels aliyefunga katika dakika 12 ya mchezo huo.