1. Afisa Viwango na Ubora wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Ndeonasia Towo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu salama inayoratibiwa na Diwani wa Chama cha Mapinduzi wa Kata ya Kipawa, Bonna Kaluwa (katikati) iliyozinduliwa katika Ukumbi wa Arnaotoglu na kilele chake kitakuwa Juni 22, mwaka huu kwenye viwanja vya Sitakishari Kata ya Kipawa, Dar es Salaam. Kampeni hiyo inalengo la kuchangisha damu ili kupunguza vifo vya wanawake wakati wa kujifungua kutokana na ukosefu wa damu.
5. Diwani wa Kipawa, Bonna Kaluwa wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo, ambapo amewahamasisha Watanzania kujitokeza kuchangia damu salama. ( Picha zote na Oscar Mbuza)
4. Diwani Bonna Kaluwa akitoa takwimu za vifo vinavyotokana na ukosefu wa damu wakati wa uzinduzi wa kampeni yake ya kuchangisha damu salama ili kuokoa vifo hivyo. Kampeni hiyo imezinduliwa Dar es Salaam leo na kilele chake ni Juni 22, mwaka huu.
3. Diwani wa Kata ya Kipawa (CCM), Bonna Kaluwa ( wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Arnaotoglu, Dar es Salaam leo kuhusu uzinduzi wa kampeni yake ya kuchangisha damu salama ili kuokoa vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu hasa vya uzazi. Kilele cha kampeni hiyo ni Juni 22, mwaka huu kwa maandamano yatakayoanzia katika viwanja vya Gonga Majumbasita hadi viwanja vya Sitakishari ambapo mgeni rasmi atakuwa Mstahiki Meya wa Ilala, Jerry Silaa.