Na Mwandishi Wetu
BONDIA Selemani Galile yupo katika mazoezi ya maandalizi ya mpambano wake dhidi ya bondia Mbwana Ally utakaofanyika February 2 katika ukumbi wa Lupinga Pub uliopo Yombo Dovya
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Galile amesema yupo fiti kwa mpambano huo kwani kwa sasa anasubiri siku ya siku tu ili aweze kufanikisha
Galile aliongeza kuwa siku hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa wakazi wa Yombo Dovya kupata burudani ya masumbwi itakayosindikizwa na mabondia chipukizi
Antony Mathias atapambana na Abuu Mtambwe huku Ramadhani Mkundi akioneshana kazi na Kassim Gamboo na Mohamedi Zungu kutoka Zanzibar atapambana na Mbena Rajabu wa Dar