Bondia Patrick kuzichapa na Class

Patrick Anthony Kavako ‘Baunsa’

BONDIA Patrick Anthony Kavako ‘Baunsa’ wa Morogoro ametamba kumchapa Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ wakati wa mpambano wao wa raundi nane utakaofanyika siku ya jumapili june 16 katika ukumbi wa panandi panandi uliopo Ilala Bungoni Dar es salaam.

Akizungumzia mchezo huo Mratibu wa mpambano huo Rajabu Mhamila ‘Super D’ alisema kuwa mpambano huo ni wa kukata na shoka ambao si wa kukosa kwani kila mmoja amejiandaa kivyake kuhakikisha anashinda mchezo huo.

“Unajua morogoro na Dar es salaam ni mahasimu katika michezo yote ukiangalia na sasa wamekutanishwa vijana katika masumbwi hivyo kila mmoja anaitaji ushindi ili ajiongezee rekodi yake kwani ‘King Class Mawe’ hato kubali kupigwa na Kavako hato kubali kupoteza mpambano wake kiraisi kwani na yeye anaitaji ajulikane katika ulimwengu wa masumbwi na kuipa sifa Morogoro kama ilivyo kwa mabondia wengine wanao tamba mkoani hapo,” alisema.
 
Mpambano huo ulioratibiwa na Kinyogoli Fondition kwa kushlikiana na PST itakuwa chachu kwa vijana kuendelea kuupenda na kuucheza mchezo huo unaopendwa na wengi nchini mbali ya mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka bondia Abuu Mtambwe ataoneshana umwamba na Kassim Gamboo na Bondia mkongwe kabisa Yohana Robart atamenyana na Mussa Sunga.
 
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali.

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo.

Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.

Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD hizo ni ya Kalama Nyilawila, Japhert Kaseba, Rashidi Matumla, Hassani Matumla, Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na Francis  Miyeyusho, Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe. 
 
mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones, Miguel Cotto, Linox Lewis, David Haye, Mohamed Ali na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D.