BONDIA Mtanzania, Omari Kimweri ‘Lion Boy’ anaechezea uzito wa light flyweight anaefanya shughuli zake nchini Australia anatarajia kupanda ulingoni mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya mpambano wake mwingine baada ya kuwatwanga mabondia kadhaa nchini humo.
Akizungumzia pambano hilo, alisema ataendeleza wimbi la ushindi kwa kutoa vipigo kama alivyotoa kwa bondia Yodpichai Sithsaithong pamoja na Lookrak Kiatmungmee ambazo ndio mechi zake za mwisho kucheza kabla ya pambano linalomkabili punde.
“…Unajua mimi ni Bingwa hivyo sito kubali kupoteza mpambano huo utakaofanyika katika ukumbi wa The Melbourne Pavilion nchini Australia.” Mpambano huo utakaosimamiwa na kamisheni ya nchi hiyo umekuwa gumzo kila kona kwa kuwa bondia Mtanzania Kimweri amejizolea umaarufu mkubwa nchini humo.
Bondia huyo aliyeanza kujishughulisha na mchezo wa ngumi za kulipwa nchini Australia mwaka 2007, Mpaka sasa akiendelea na shughuli zake hizo amesema lengo lake kubwa ni kutwaa mikanda inayotambulika kimataifa ingawa yeye kwa sasa ni bingwa wa WBO, ubingwa alioupata kwa kumtwanga bondia Panmongkol Ekarin wa Thailand.
Bondia huyo amewaomba watanzania kumuombea duwa kwani ana kibarua kizito cha kuitanganza nchi yake kimataifa bondia huyo mwenye uraia wa nchi mbili Tanzania na Austalia amesema ana mpango wa kuja Tanzania na kuzamini mchezo huo kama mfadhili endapo malengo yake yatatimia.
“…Mimi nataka nije kupigana Tanzania nikiwa mchezaji na promota vile vile hivyo nafanya mpango huo mambo yakiwa mazuri nitakuja bongo ili nifanye uwekezaji katika Boxing,” alisema.
Bondia huyo mpaka sasa amekwisha cheza mapambano 15 akishinda 12 na kupoteza mapambano matatu bondia huyo anayefananishwa na Simba muwindaji amekuwa tishio kwa mabondia wenye uzito wake kwa niaba ya watanzania wote tunaungana kumsapoti bondia Omari Kimweri anayefanya kazi zake nchini Austalia aweze kushinda mpambano waku huo Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri, AMIN