Bondia Maarufu wa Kike Kuzichapa Septemba 26 Ujerumani

female prof.boxer Bintou Yawa Schmill

female prof.boxer Bintou Yawa Schmill

The Voice Boxer Bintou Schmill.

The Voice Boxer Bintou Schmill.

BONDIA maarufu wa kike Mwafrika barani Ulaya, Bintou Yawa Schmill a.k.a “The Voice” anatarajiwa kupanda ulingoni Septemba 26, 2014 kupambana na bondia Mirjana Vujic katika ukumbi wa Stadthalle/ Saalbau Frankfurt-Nied, Mjini Frankfurt ujerumani.

Bintou Yawa Schmill “The Voice” mzaliwa wa Togo ambaye anapigania uzito wa Welterweight – 64, urefu mita 1.71 historia yake alikuwa bondia wa ngumi za ridhaa kwa muda miaka mitano, kuanzia mwaka 2007 na baadaye aliingia katika ngumu za kulipwa. Amecheza mara 8, ameshinda michezo 7 kwa K.O.s.

Bondia Bintou Yawa Schmill juzi katimiza umri wa miaka 30, na ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Bremen na ndiye aliyelipamba jarida maarufu la warembo “Penthouse”. Bondia huyo wa kike anayeliwakilisha bara la Afrika Ughaibuni mara nyingi amefananishwa na Simba (Bintou is the Lioness), ambaye ukimuona mpishe njia ulingoni.

Bintou “The Voice” Schmill sasa kapania kuweka rekodi ya kuwachapa wapinzania wake kila kona duniani ! Mengi kuhusu bondia Bintou Schmill aka ‘The Voice” usikose at; http://www.facebook.com/schmillbintou but first all visit the lion queen on http://www.bintou-schmill.de/also http://www.twitter.com/schmillbintou