BONDIA Bora wa mwaka 2013/14 katika uzito wa KG 63, Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ ame saini mkataba wa kupambana na Cosmas Cheka Feb 8, 2014 katika ukumbi wa PTA uliopo Sabasaba jijini Dar es Salaam. Mara baada ya kusaini mkataba huo wa kucheza raundi 10 za ubingwa wa Taifa Kg 60 alisema atafanya mazoezi ya kutosha kuhakikisha anamkung’uta mpinzani wake raundi za awali kwa kuwa bondia huyo amekuwa akichonga sana juu yake.
Mpambano huo uliodhaminiwa na Promota Jay Msangi utakuwa na msisimko wa aina yake kutokana na mabondia hao kuwa gumzo katika ulimwengu wa masumbwi ndani ya Tanzania. King Class aliongeza kwa kusema kuwa nipo fiti nimejiandaa na ninasubili tu kuvishwa ubingwa huo wa taifa kwani Cheka ana ujanja kwangu mbinu zake zote nimesha zikamata.
King Class Mawe anafanya mazoezi chini ya jopo la makocha wanao ongozwa na Habibu Kinyogoli ‘Masta’ Rajabu Mhamila ‘Super D’ na Kondo Nasoro. Bondio huyo amewashukuru wadau wa mchezo wa ngumi kwa kumuwezesha kuchaguliwa kuwa bondia bora wa mwaka katika uzito wake kwa kuwapita mabondia wengine wanne na yeye kuibuka kidedea katika kinyang’anyiro hicho.