Bondia Herbert Quartey na Albinus Felesianu Kuzichapa Machi 29

Bondia Herbert Quartey na Albinus Felesianu Kuzichapa Machi 29

MABONDIA kinda Herbert Quartey kutoka Ghana na Albinus Felesianu wa Namibia wanatarajia kuwania Ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito wa Super Feather watakapokutana Machi 29, mwaka huu jijini Windhoek, Namibia. Huu ni mpambano ambao utawakutanisha kinda wawili ambao wana usongo wa kuendeleza rekodi ya ngumi utakaowafungulia mlango kwenye ubingwa wa watu wazima.

Hii inakuja katika kipindi kisichozidi wili mbili katika ukumbi wa hoteli ya Windhoek Country Club and Casino iliyoko nje kidogo mwa jiji la Windhoek baada ya mpambano mwingine wa IBF kati ya Immanuel “Prince” Naidjala na Lesley Sekotswe wa Namibia kugombea mkanda wa IBF wa Kimataifa ambako walitoka ngoma draw.

Mpambano kati ya Albinus na Herbert unaandaliwa na promota maarufu nchini Namibia Kinda Nangolo wa kampuni ya Kinda Boxing Promotionsambaye pia anatamba kuwa na bingwa mwingine wa IBF katika uzito wa Feather Gottlieb Ndokosho. Bwana Kinda anataka kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye ndiye promota maarufu zaidi katika ngumi za kulipwa katika ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mpambano huo umeidhinishwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika na litasimamiwa na Rais wa shirikisho hilo Mtanzania Onesmo Ngowi ambaye yuko jijini Accra, Ghana ambako jana usiku alisimamia pambano la ubingwa wa Afrika katika uzito wa welter kati ya Frederick Lawson na Isaac Sowah wote wa Ghana lililofanyika katika uwanja wa mpira wa Accra.