Bondia Francis Cheka Sasa Kuzipiga na Simon wa Ujerumani

Bondia Benjamin Simon wa Ujerumani


Bondia Francis Cheka wa Tanzania akiwa mazoezini

PAMBANO la ngumi kati ya bondia Francis Cheka kutoka Tanzania na Benjamin Simon wa nchini Ujerumani linalosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa mchezo wa ngumi sasa litafanyika Novemba 18, katika Ukumbi wa Universal jijini Berlin Ujerumani.

Awali mpambano huo ulikuwa ufanyike Novemba 17 jijini Berlin, Ujerumani na tayari bondia Francis Cheka ameshasaini mkataba wa kukutana na mbabe huyo wa Ujerumani anayejulikana kwa jina la “Iron Ben” kwa ajili ya ukali wa makonde yanayowasulubu wapinzania wake.

Bondia Benjamin Simon ana rekodi ya mapambano 24 ambapo amepoteza pambano moja wakati bondia Francis Cheka ana rekodi ya mapambano 33 amepoteza mapambano sita. Akimwandikia “Eva Rolle” wa kampuni ya “Primetime Event Management” ya Ujerumani ambaye ndiye promoter wa mpambano huo, Mwenyekiti wa Ubingwa wa IBF/USBA Lindsey Tucker alimfahamisha kuwa Rais wa IBF/USBA Daryl Peoples au yeye mwenyewe Lindsey Tucker watawasiliana na mama huyo kuhusu maofisa watakaosimamia mpambano huo.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa wababe hao kukutana kugombea mkanda wa IBF wa mabara (IBF I/C) na mpambano wao unategemnea kutoa ushindani mkubwa. Mshindi katika mpambano huo ataingia moja kwa moja katika orodha ya mabondia 15 bora kwenye uzito wa Super Middle duniani.