KAMERA ya dev.kisakuzi.com jana imeshuhudia nyumba za zilizokuwa kota za Shirika la Reli Tanzania na zile za bandari eneo la Kariakoo Gerezani zikivunjwa na tigatiga chini ya ulinzi mkali wa askari polisi pamoja na vijana wa Kampuni ya udalali ya Majembe.
Kwa mujibu wa mashuhuda wanasema nyumba hizo zilianza kuvunjwa kuanzia usiku wa kuamkia jana majira ya saa kumi chini ya ulinzi mkali wa polisi pamoja na vijana wa Majembe. Taarifa za mashuhuda zinasema nyumba hizo zimevunjwa baada ya kesi ya wamiliki wa nyumba hizo kutupiliwa mbali hivi karibuni. Eneo hilo Serikali imepanga kujenga kituo kikuu cha mabasi yaendayo kasi ya jijini Dar es Salaam. Zifuatazo ni picha mbalimbali ya uvunjaji wa eneo hilo;