Hivi ndivyo kituo cha daladala cha Mwenge kilivyo bomolewa asubuhi ya leo.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa.
Kazi ya kubomoa na kuondoa vibanda ikiwa inaendelea Mwenge.
Askari wa FFU akiwa anazuia watu wasipite eneo ambalo kulikuwa na kazi ya bomoa bomoa ikiendelea.
Mashuhuda wakiwa wanashuhudia ubomoaji ukiendelea.
Hili lilikuwa eneo la kupumzikia zamani la Abiria kungoja usafiri nacho kikiwa kimebomolewa.
Mabaki ya Vibanda
Mmoja wa mgambo akiwa amebeba meza kupeleka eneo husika tayari kwa kuzikusanya kuzipeleka eneo husika.
Kazi ya ubebaji meza na mabaki ya vibanda ikiendelea.
Mashuhuda wakiongezeka.
Moja ya eneo ndani ya Mwenge walipo hifadhi baadhi ya meza za biashara.
Bomoa bomoa ikiendelea upande wa juu Mwenge.
Hapa walikuwa wanabomoa sehemu zote za vibanda zilivyo zidi mbele.
Mgambo anafanya kazi bila Air Mask wakati kazi inaendelea ya Bomoa bomoa
Mashuhuda upande wa juu Mwenge.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa kila sehemu.
Hapa ilitaka kutokea shoti ya umeme baada ya gari la kubomoa kupita sehemu ambayo kuna waya wa umeme, TANESCO hawajazima umeme eneo hilo jambo ambalo ni hatarishi.
Hali Halisi baada ya eneo hilo kubomolewa. Chanzo Dar es Salaam Yetu Blog.