Boko Haram Wazuia Watu Kuzika Ndugu Zao

Maasi ya Boko Haram nchini Nigeria

Maasi ya Boko Haram nchini Nigeria

SENETA wa mjini Bama nchini Nigeria, Ahmed Zanna amesema kwamba wakazi wa eneo hilo wamezuiwa kuwazika jamaa zao waliouawa na wapiganaji wa Kiislam wa Boko Haram. Taarifa zaidi kutoka Mji wa Bama ikiwa ni miongoni mwa miji iliyotekwa na wapiganaji wa Kiisilamu wa Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, wamezuiwa kuwazika ndugu zao waliouwawa.

Taarifa za kina zinasema hivi sasa miili imetapakaa katika barabara za mji huo ambao Boko Haram imeuteka na hakuna anayezika kwa kuhofia maisha yake. Kundi hilo linasemekana kuuteka mji huo huku wapiganaji wa kundi hilo wakishika doria katika barabara zake.

Maelfu ya watu wametoroka huku idadi kubwa ya wengine wakiuawa. Seneta huyo ameitaka serikali ya Nigeria kupeleka wanajeshi mjini Maiduguri ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo ili kuulinda dhidi ya wapiganaji hao. Mnamo siku ya Jumatano serikali ya jimbo hilo ilikanusha madai kuwa jimbo hilo limetekwa na wapiganaji hao.

Maofisa wakuu wanakisia kuwa watu 26,000 wameachwa bila makao kutfuatia mapigano katika mji wa Bama.
Bwana Zanna anasema kuwa barabara za mji huo zimejaa miili ya watu na Boko Harama imewakata wakazi kuwazika jamaa wao. “Kwa hivyo hali ni mbaya na inaendelea kuzorota,” asema Zanna.

Boko Haram wameteka miji kadhaa Kaskazini Mashariki ya Nigeria, katika miezi ya hivi karibuni na kusababisha hofu kuwa huenda wakaufikia mji mkuu Maiduguri. Bwana Zanna amesema kuwa itakuwa janga kubwa ikiwa Boko Haram wataushambulia mji wa Maidiguri ambao una watu zaidi ya milioni mbili.

-BBC