Boko Haram Wateka Vijiji Wauwa, Nigeria Hakuna Ebola…!

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan

WATU wanaohisiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram, wamewapiga risasi na kuwachinja watu katika vijiji vitatu Kaskazini Mashariki mwa Nigeria licha ya serikali kudai mwishoni mwa wiki kuwa ilifikia makubaliano na kundi hilo.

Wapiganaji wa Boko Haram, walivamia vijiji viwili Jumamosi na kupandisha bendera yao kwa mara ya tatu. Hii ni kwa mujibu wa wanakijiji wa eneo hilo. Serikali ilisema kuwa itaendelea kufanya mazungumzo na Boko Haram licha ya madai ya kundi hilo kuvunja makubaliano.

Inatumai kuwa kundi hilo litawaachilia zaidi ya wasichana miambili waliowateka nyara amwezi Aprili. Boko Haram hawajasema chochote kuhusu tamko la serikali ya Nigeria Ijumaa kwamba wamekubali kusitisha vita na kuwaachilia wanafunzi hao miambaili waliotekwa nyara katika eneo la Chibok.

Inaarifiwa Boko Haram wanawakilishwa kwenye mazungumzo ya upatanishi yanayofanyika nchini Chad na Danladi Ahmadu. Hata hivyo, duru zinsema mwakilishi wa kundi hilo ni mtu bandia asiyetambulika na Boko Haram. Hatua ya serikali kushindwa kuwaokoa wasichana hao imesababisha maandamano nchini Nigeria. Wasichana hao walipotekwa nyara dunia nzima ilishtuka na hata kuanzisha kampeini ya kutaka serikali kuwaokoa wasichana hao.

Wakati huo huo; Shirika la afya duniani limetangaza rasmi kuwa taifa la Nigeria halina ugonjwa wa Ebola, wiki sita baada ya kutoripotiwa kwa visa vya ugonjwa huo. Nchi hiyo yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, lipokea sifa tele kwa hatua zake za haraka kukabiliana na Ebola baada ya mwanmadiplomasia Mliberia mwenye ugonjwa huo kwenda Nigeria mwezi Julai.

Shirika la afya duniani lilitangaza Senegal kutokuwa tena na Ebola mnamo siku ya Ijumaa.
Mlipuko unaoshuhudiwa wa Ebola, umewaua watu 4,500 katika kanda ya Afrika Magharibi hasa nchini Liberia, Guinea na Sierra Leone. Inakisiwa asilimia 70 ya wale walioambukizwa ugonjwa huo wamefariki katika mataifa hayo.

Shirika la afya duniani linaweza tu kutangaza nchi kutokuwa na Ebola ikiwa siku 21 zitapita bila ya kuripotiwa kwa visa vipya vya Ebola. Kisa cha mwisho kilichoripotiwa cha maambukizi mapya ya Ebola, kiliripotiwa tarehe 5 Septemba. Janga hilo, lilianza kuripotiwa,wakati raia mmoja wa Liberia kuripotiwa kuwa na Ebola mwezi Julai.

Nigeria ilitangaza hali ya tahadhari kiafya huku bwana Sawyer akifariki baadaye kutokana na ugonjwa huo pamoja na raia wengine saba wa Nigeria. Raia hao walikuwa pamoja na Daktari Ameyo Stella Adadevoh, aliyetambua kuwa Sawyer alikuwa na Ebola na alisifika kwa kusaidia katika harakati za kudhibiti ugonjwa huo.

Balozi wa Liberia alipeleka virusi vya ebola mjini Lagos mwezi Julai. Alikuguliwa kuwa na Ebola hospitalini alipofanyiwa uchunguzi wa awali. Mkurugenzi wa hospitali hiyo Daktari Benjamin Ohiaeri, amesema kuwa mlipuko huo umekuwa na athari kubwa.

Mawaziri mambo ya nje wa muungano wa ulaya wanakutana kujadili mikakati ya kudhibiti maambukizi ya ebola. Zaidi ya watu 4500 wamekufa kutokanma na mlipuko wa ugonjwa huo wengi wao raia wa Afrika Magharibi.
-BBC