Boko Haram Kuwauza Wasichana Iliyowateka, Polisi Watumia Fedha Kuwasaka

Polisi nchini Nigeria

Polisi nchini Nigeria

KUNDI la Boko Haram limekiri kuwateka nyara wasichana wa shule moja nchini Nigeria na limesema kuwa linajiandaa kuwauza. Polisi nchini Nigeria wameahidi kumtunuku dola laki tatu za marekani yeyote atakayetoa habari zitakazowasaidia kuwapata zaidi ya wasichana mia mbili waliotekwa na kundi la wapiganaji wa boko haram mwezi uliopita.

Juma lililopita wapiganaji wa Boko Haram walisema kuwa wasichana hao 200 kutoka eneo la Chibok waliotekwa mwezi uliopita watauzwa. Aidha Maofisa nchini Nigeria walisema kuwa idadi ya wasichana zaidi waliotekwa nyara na kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram imetimia 11, licha ya Boko Haram kutangaza kuwa ni 200.

Polisi ilisema wasichana nane kati yao walitekwa kutoka Kijiji cha Warabe kilichoko katika Jimbo la Borno siku ya Jumapili na watatu zaidi wakatekwa kutoka kijiji jirani na hicho. Rais wa Marekani ameingilia suala hilo akisema kuwa serikali yake itatoa msaada ili kuwakomesha wapiganaji hao.

Tayari Marekani imewatuma maofisa kadhaa kusaidia kusuluhisha kwa amani kitendawili cha utekaji nyara huo.
-BBC