Msajili wa Bodi ya wahandisi nchini Mhandisi Steven Mlote akijibu maswali ya waandishi habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano baina yao uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kwa mwaka wa fedha 2011/12 Bodi hiyo iliweza kuwafutia usajili wahandisi 164 ambao walikiuka maadili ya kazi na kusimamisha miradi 12 kutokana na ukiukwaji wa kanuni za uhandisi na taratibu za kiujenzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Prof. Ninatubu Lema. (Picha na Anna Nkinda-Maelezo Dar es Salaam)