Bodi MSD Yawavua Ukurugenzi Waliosimamishwa na Waziri

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (Mb.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (Mb.

BODI ya Wadhamini ya Bohari ya Madawa nchini (MSD) imewavua ukurugenzi wakurugenzi wawili waliosimamishwa kazi hivi karibuni na kumfukuza kazi mmoja baada ya kukutwa na makosa kwenye uchunguzi uliofanywa juu ya tuhuma mbalimbali dhidi yao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Laurean Bwanakunu jijini Dar es Salaam inasema waliovuliwa ukurugenzi ni Bw. Joseph Tesha na Misanga Muja aliyekuwa Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD.

Taarifa inasema Bw. Cosmas Mwaifwani ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wajeja, ambaye pia alisimamishwa kupisha uchunguzi amepatikana na kosa hivyo amefukuzwa kazi kuanzia Julai 8,2016 kwa kufuata sheria na kanuni za SMD.

Taarifa ya Bwanakunu inasema Bw. Heri Mchunga ambaye ni niongoni mwa maofisa waliosimamishwa ameonekana hana hatia hivyo amerudishwa kazini na kuhamishiwa Kurugenzi ya Ugavi kushika nafasi ya Mkurugenzi.