Kampuni mbili kubwa duniani za kuunda magari, zimeamua kushirikiana kiufundi, na kutengeneza magari ambayo hayatachafua sana mazingira. Toyota na BMW walitangaza ushirikiano huo wao mpya nchini Japan, siku chache kabla ya maonyesho ya magari kufunguliwa rasmi nchini humo.
Kati ya mipango yao ya pamoja ni kutengeneza betri bora zaidi kutumika katika magari yanayotumia umeme.
Makampuni mawili yanayoongoza kwa utengenezaji wa magari duniani yanawekeza kiwango kikubwa cha fedha kuunda magari ambayo yanaafikiana na mahitaji ya mazingira masafi.
Makampuni hayo imebidi yafanye hivyo, kwa sababu serikali sasa zimezidi kuhimiza kubaini malengo ya matumizi ya kadri ya mafuta pamoja na wasiwasi juu ya uhariubifu wa mazingira kukiwa na ongezeko la joto duniani na wanunuaji wa magari wanaozidi kufahamu kuhusu mazingira.
Lakini gharama za utaalamu unaohitajika katika kuunda magari yanayokubalika kuambatana na mazingira bora ni kubwa hata kwa mabwanyenye wa viwanda kama hivyo, iki9maanisha kuna shinikizo kwa watengeneza magari kua na ushirikiano na washindani wao.
Ushirikiano kama uliofikiwa baina ya Toyota na BMW ni sehemu ya ushirikiano wa aina hiyo katika kuharakisha mchakato wa maendeleo kufikia teknolojia ya magari kwa wepesi. Labda kigezo kikuu kitakua kuundwa kwa Betri bora kwa magari yanayotumia umeme na umeme -sehemu kuu katika makubaliano baina ya BMW na Toyota.
Na kama alivyowaelezea wandishi wa habari mjini Tokyo msemaji wa kampuni hiyo Klaus Draeger alisema kuwa
“katika siku za usoni kampuni ya BMW pamoja na kampuni ya Toyota Motor Corporation zitashirikiana katika kilichoundwa kua ushirikiano wa mda mrefu. Kwa kufanya utafiti kwa pamoja tunataka kuunda tekonolojia ya Betri kwa haraka.”
Kwa kipindi cha mda mrefu ujao Makampuni haya mawili yatatengeneza muundo mpya wa Betri za lithium za magari. Kampuni ya Toyota imekua ikikumbwa na matatizo ya Betri zinazotumiwa katika magari yake aina ya Prius.
Teknolojia inayofanyiwa majaribio imeisha tumiwa kwa mda katika vifaa kama vile cameera na simu za mkononi na kwa bei nafuu ingawa juhudi za kuongezea nguvu na ukubwa kwa ajili ya magari umekuwa mtihani mkubwa kufikia bei inayokubalika.
-BBC