JUMATANO iliyopita tarehe 19 Mei 2013 kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, timu pinzani kutoka barani Afrika zilipambana kushindania nafasi mbili za fainali ya mashindano ya Pan-African Guinness Football Challenge. Walikuwa ni kutoka Ghana Emanuel Kofi Okarku na Isaac Aryee ambao kwa mara nyingine walianikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness.
Wakenya katika jezi nyekundu Keneth Muturi na Chris Mwangi walikuwa ni wa kwanza kutoka baada ya kuwa alama chache zaidi ya timu zingine na kuwa wa mwisho katika mzunguko wa kwanza wa mchezo. Matumaini ya Afrika mashariki yalirudi baada ya timu nyingine ya Kenya kukusanya alama 14 katika mzunguko wa pili na kufikia hadi mzunguko wa penati baada ya kuishinda timu ya Cameroon. Mzunguko wa penati ulikuwa ni mgumu kwa kuwa timu hizi hazikuachana sana lakini muda ulipokwisha waghana walishinda na kujipatia dola za kimarekani 4,500 katika hatua ya ukuta wa pesa wa Guinness.
Emmanuel na Isaac watakutana na Waghana wenzao katika fainali pamoja na washindi wa pili kutoka Afrika mashariki ambao ni Francis Ngigi na Kepha Kimani na Ephatua Nyambura na Samuel Papa. Wote wana nafasi ya kupeperusha bendera za nchi zao lakini watahitaji kujiandaa vizuri ili waweze kuwa washindi wa mashindano haya ya Guinness Football Challenge.
“Timu zote katika mashindano haya tangu mwanzo zimefanya vizuri na timu hizi nne za mwisho zinastahili nafasi ya fainali.Wiki ijayo kutakuwa na mpambano baina ya Afrika mashariki na Afrika magharibi huku kila upande ukiwa na timu mbili. Tungependa kuwaomba watu wote kutoka Tanzania Uganda na Kenya kuangalia mchezo huu na kushangilia timu za Afrika mashariki kuleta taji nyumbani. Timu zote sasa zitatakiwa kuonesha ujasiri watakapopambana katika fainali ya kwanza kabisa ya Pan-African Guinness Football Challenge! Usikose kuangalia mchezo huu – hakika itakuwa ni fainali ya kusisimua,” alisema Meneja wa kinywaji cha Guinness, Davis Kambi.
Wakali waliotinga fainali za Pan-Afican Guinness Football Challenge:
AFRIKA MASHARIKI:
• JEZI ZA KIJANI – kutoka Kenya watakuwa ni Ephatus Nyambura (24) na Samuel Papa (23). Wtakuwa na matumaini ya kushinda zaidi ya dola za kimarekeni 3,000 walizopata katika hatua za mwanzo.
• JEZI NYEKUNDU – Timu ya pili kutoka Kenya ya Francis Ngigi (23) na Kepha Kimani(25) kutoka Thika.Timu hii mpaka sasa imejishindia dola za kimarekani 3,000 na wana matumaini ya kushinda katika fainali.
AFRIKA MAGHARIBI:
• JEZI NYEUSI – Emmanuel Kofi Okarku (27) na Isaac Aryee (25) kutoka Ghana wataichezea timu yao kutoka Afrika magharibi.Tayari wamejishindia dola 7,000 na wanatarajia kufanya vizuri zaidi katika fainali.
• JEZI ZA BLU – Wakubwa walioshinda pesa nyingi zaidi mpaka sasa ambao ni Jonathan Naab (25) na Desmond Odaano (26) kutoka Larteh wameshinda hadi dola 20,000.Ni kiasi kikubwa je watafanya vizuri zaidi katika fainali?
Ushindani baina ya Afrika mashariki na Afrika magharibi utakuwa ni mkali, nani atakaeibuka mshindi?
Fainali ya Pan-African Guinness Football Challenge inatayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol na kurushwa katika televisheni ya ITV na Clouds TV Jumatano saa 3:15 usiku ITV na saa 2:15 usiku Clouds TV. Usikose kushuhudia timu kutoka Afrika Mashariki ikipambana vikali na nchi zingine za Afrika.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness football challenge barani Afrika wanaweza kupima maarifa yao katika kabumbu kupitia GUINNESS® VIP™. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.
Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.