MI wakati mwingine huwa siwaelewi wana siasa wa nchi hii!! Yaani sasa kazi yao kubwa imekuwa ni kuteka hisia za wananchi eti kwa kusudi la kuonekana wao wema dhidi ya upande mwingine. Hili linanikera sana mimi, kwa sababu sasa badala ya kutumia muda kujadili masuala ya maendeleo ya Mtanzania, wamekuwa wakitumia fedha za wananchi na rasilimali za nchi kuendekeza mijadala na marumbano ya kisiasa, huku maslahi ya vyama vyao yakiwekwa mbele kuliko maisha ya Mtanzania anayeishi katika maisha magumu! Kiukweli, hadi sasa, mimi sijaona mwana siasa ambaye kwa dhati anataka kulifaidia TAIFA.
Ikiwa yupo, itakuwa ni yule ambaye anawaza, Nikijifanyia hiki, na kile, na familia yangu, na jamaa zangu, kisha nitafafanya hivi,…. kwa ajili ya TAIFA. Maneno ya mtunzi wa kitabu, The Beautiful ones are Not yet born” bado yanaendelea kuwa na ukweli hasa kwa siasa za Tanzania. Nitakuambia, kwa nini hoja yangu ina mantiki.
Hembu kama si uchu wa madaraka walio nao wana siasa, wakae chini kwa upendo wakati wanapotaka kusimamisha mgombea yeyote, kisha mtu asipige kampeni ya kuchaguliwa, bali wanachama wenyewe wawe wanapendekeza kuwa fulani anastahili kututumikia katika nafasi fulani, wasifu wake utolewe, kisha watu wapige kura kumchagua, siyo yeye atumie pesa nyingi kwenda kujitangaza mwenyewe kuwa anafaa na kuwalaghai watu.
Nina ujasiri wa kusema kuwa wana siasa walio wengi kama si wote, huwa wanatathimini keki iliyo pale juu, ndo mate yanawadondoka kama mbwa anavyofanya wakati anapoona mnofu kama Avogadro alivyowafanyia majaribio. Kinachofuata baada ya mate kuwatoka ni kuazimia kufanya kila liwezekanalo ili mradi tu afike kwenye keki na kuitafuna. Mfano mzuri uko huku vyuoni katika elimu ya juu, ambako kuna vijana wengi tena wanaojifanya kuwa wana uchungu na rasilimali za nchi.
Pindi inapofika uchaguzi wa serikali za wanavyuo, utakuta mtu anaanza mapema kampeni za kugombea, huku akiwa ameandaa fedha nyingi ama kwa kukopa, ama kwa kulimbikiza ili mradi tu aweze kuteka kundi kubwa la watu wakati wa uchaguzi. Sasa mi huwa najiuliza, utakuta mtu katoka jasho na misuli, ati anataka Uraisi ili akatumikie wana chuo, kazi haina mshahara ila yeye anawekeza pesa nyingi kwenye mradi huo, hadi za kukopa.
Atapataje pesa za kurudisha, mimi na wewe hatujui! Sasa itokee ameukosa uraisi, weeee!! movement zitaanzishwa hapo, oh wamenichakachua, mara hivi!! Kumbe mradi aliowekeza pesa nyingi umeingia hasara. Sasa njoo kwa yule aliyekitata kiti, wanafunzi tutachangia mfuko wa Serikali kwa milioni zaidi ya mia moja, chuo kitatoa ruzuku zaidi ya milioni mia, lakini mwisho wa uongozi wake, hakuna hata senti inayobaki, hakuna mchanganuo wa jinsi pesa ilivyotumika, hakuna kitu cha kuonekana kilichofanyika kwa pesa hizo zaidi ya kuona watu wakinunua magari, wakijenga nyumba n. k.
Hii inatuambia nini kuhusu mstakabali wa TAIFA letu hasa kuhusiana na Uaminifu wa wale wanaoendelea kupikwa kisiasa ili wawe viongozi wa kesho? Na ni hawa hawa ndo ambao kesho baada ya kumaliza vyuo tunawakuta kwenye majukwaa ya kisiasa eti wakisema kuwa wao ndo wanastahili kushika dola, wapi! huu ni unafiki na ulaghai!! Wamekwishafanya mazoezi ya kuiba keki ya Taifa tangu wako huko katika jumuia ndogo sasa wanataka ku-exercise wizi wao katika ngazi za juu zaidi.
Na hii haijalishi kuwa mtu yuko katika chama gani cha siasa, ama ni upinzani, au ni chama tawala, wote ni sawa. Na hapa ndo nataka kuhitimisha kuwa, There is no correlation between the name of political party and the political candidate in terms of quality of leadership and behaviour. A good behaviour is a result is an outcome of the long nurturing process that takes place in the society from which an individual comes from. Kwa hiyo napenda kuwaasa Watanzania wenzangu kuwa, tunapomtathimini mtu kuhusu ubora wake katika nafasi za uongozi, yatupaswa tuwe na uwanja mpana wa kufanyia tathimini usiofungwa na mipaka ya kichama na siasa.
Haya ni maoni ya msomaji wa Thehabari.com
Amejitambulisha kama; Bw. Kasase (hamenyas@gmail.com)