KAMPUNI changa ya Bigright Promotion inaanzisha mkakati wa kuwapiganisha mabondia kuwania mikanda au kutetea mikanda yao isipotee. Taarifa hiyo imetolewa na Ibrahim Kamwe ambaye ni kiongozi wa kampuni hiyo. Kiongozi huyo alisema wataanza kuandaa ubingwa wa mapambano ya uzito mdogo yaani light fly weight, baadae kuandaa fly weight na super fly, bantam na heavy weight.
“Hii itawasaidia mabondia kupata mapambano ya mara kwa mara na kuwapatia kipato kidogo kwa ajira walioichagua inayoambatana na utambulishaji wa kimataifa kwa nchi yetu, kwani mchezo wa ngumi ni mchezo mmojawapo unaoutangaza na kuipeperusha vema bendera ya nchi yetu kimataifa…bila ya Watanzania wengi kulifahamu hilo na kukosa usaidizi mzuri toka Serikalini na taasisi binafsi tofauti,” alisema.
Alisema baadhi ya nchi za wenzetu zinazopenda na kuithamini michezo, Nchi nyingi zinatangazika kupitia michezo hadi sisi tunazifahamu na kuzitembelea au kuwa na shauku ya kutaka kuzitembelea, wakati uwezo huo wa kufanya vizuri tunao lakini hatusaidiwi kujinyanyua wala kuwa na sehemu ya kueleweka kwamba hii ni kwa ajili ya ngumi (ulingo wa kisasa na ukumbi wa uhakika), na wakati wadau wa mchezo huu tunanung`unika na kuhaha kutafuta wadhamini nasi tujikwamue tokakatika hali tuliyonayo, kuna wengine wasio wastaarabu watataka kuchukua nafasi hii kufanya ubadhilifu dhidi ya wanaosaidia-hii sio njema na inadumaza michezo.
“Kwa mfano mashindano yaliyo andaliwa na bigright tarehe 7 Aprili Mwananyamala hayana udhamini wala ufadhili wowote hivyo yanaendeshwa katika hali ya ugumu ili vijana nao wapate kucheza kuliko kufanya mazoezi ya muda mrefu bila mashindano hivyo kuwasababisha baadhi ya mabondia kukata tama na kuacha ngumi au kijiingiza katika vitendo vya ukabaji jambo ambalo sio jema na laweza kuepukika kwa kuwaandalia mashindano kama haya na ili azma yetu ya kuyafanya yaendelee yatubidi tushirikiane kwa kushawishi wafadhili,”
“…Wadhamini au wapenda mchezo wenye uwezo kidogo wawe wanatuwezesha japo kidogo walichonacho ili nasi tuwe tunaongeza nguvu ya kupigania michezo isidorole, mipango ikienda kama tulivyopanga tunategemea kila mwezi kuwashindanisha kugombania ubingwa na kila mwezi wa 12 kunakuwa na ligi ya mabingwa na kumzawadia mshindi kitu ambacho atakuwa anakikumbuka katika maisha yake, hivyo kwa alie tayari na mwenye mapenzi na maendeleo ya michezo tunaomba mchango wako uwe wa vifaa kama gloves, bandages, ballguard, headguard, gumshield, chakula, nauli, ulingo na mengineyo mengi tu sijayaorodhesha, msitutenge na uwezo wetu mdogo tusaidiane,” alisema Kamwe.