Bigright awakomalia vijana mchezo wa ngumi

Vijana wadogo wa timu ya ngumi ya Bigright boxing wakiwa katika pozi la pamoja na kiongozi wao Ibrahim 'bigright' (mwenye miwani na fulana nyeusi).

IBRAHIM Kamwe ‘bigright’ ambaye ni promota wa ngumi ameamua kuwafundisha vijana wadogo mchezo wa ngumi ili waje kuwa wachezaji wazuri wa mchezo huo hapo baadaye. Akizungumzia hatua hiyo, Ibrahim anasema; “Mabondia wengi hapa nchini wanapigana ili mradi wanapigana hawana formula zozote, hawajui kujilinda pale wanapoelemewa, hushambulia kwa kubahatisha tu, pia hawajui sheria za mchezo wenyewe yote kutokana na kukurupukia mchezo ukubwani.”

Anasema baadhi ya mabondia wamekuwa wakikurupuna na pale wanapofanya maandalizi kidogo unakuta wanatafuta pambano, na wanapopata mchezo mmoja au miwili basi anakuwa hakubali kukosolewa kila kitu anajiona anajua jambo ambalo linawafanya wengi kuwa na upungufu mkubwa kimchezo huo.

“Wanasema ‘SAMAKI MKUNJE YUNGALI MMBICHI’ na si baadaye tunailalamikia Serikali. Sisi tujitahidi ili tuiamshe Serikali itusaidie, sababu inatulazimu kujua kama Serikali yetu imelala katika michezo mingine ambayo pia ndiyo inayoleta ushindi na sifa ulimwenguni,” anasema mtaalamu huyo wa ngummi.