Bia ya Tusker Yazinduwa Shindano la ‘Tusker Project Fame’

Meneja wa Bia ya Tusker kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti, Sialouise Shayo (katikati) akizungumza na wanahabari leo kuhusu  TUSKER PROJECT FAME. Kushoto ni Meneja Masoko Tusker, Anitha Msangi na  msanii mahiri Zahira Zoro.

Kutoka kushoto ni Anitha Msangi,  Sialouise Shayo, Mwanamuziki mahiri Zahira Zorro, na mzao wa Tusker Project Fame, Aneth Kushaba.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.

Mkutano na waandishi wa habari

TUSKER PROJECT FAME IMERUDI TENA!

KWA miaka 7 sasa TUSKER PROJECT FAME imeendelea kuwapagawisha mashabiki wake Afrika Mashariki huku ikiwa na washiriki wengi kutoka Tanzania ambao hufanya vizuri mashindano hayo. TUSKER PROJECT FAME imerudi tena kwa kishindo na mwaka huu ikiwa ni msimu wa 6 wenye muonekano wa kipekee kwani mashindano haya yameboreshwa na kupanua wigo wake ambapo washindi katika usaili wataweza kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la Tusker project fame nchini Kenya na mshindi ataweza kujishindia shilingi milioni 100 za kitanzania na kuingia mkataba wa kurekodi wa shilingi milioni 200 za titanzania.

Akiongea na wana habari, Meneja wa bia ya Tusker kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti Sialouise Shayo amesema “Tunawakaribisha watanzania wote ambao wanaamini wanakipaji na wanaweza kudhihirisha kuwa kweli wao ni nyota katika muziki. Ili waweze kujipatia nafasi ya kushiriki watanzania wanaweza kuudhuria usaili utakaofanyika tarehe 7 na tarehe 8 Septemba katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam. Vigezo na masharti vitazingatiwa na wanachotakiwa kufanya ni kuwapagawisha majaji na kuwaonyesha kuwa kweli mshiriki anaweza kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano”.

Mashindano haya yatatikisa zaidi kwani Mwanamuziki mahiri Zahira Zorro atakuwa jaji katika mashindano haya. Yeye na majaji wenzake wataanza katika usaili. Tanzania mwaka huu itapata nafasi ya kuwakilishwa na washiriki wenye uwezo wa kujiamini kwa hali ya juu. Mashindano hayo yataoneshwa katika televisheni inayoongoza kwa burudani Afrika Mashariki, East Afrika Television (EATV)

“Najivunia na najiona mwenye bahati kuwa miongoni mwa majaji watakaohakikisha vipaji stahiki vinang`ara na kuiwakilisha nchi yetu. Kwangu hii ni fursa kwa kuhakikisha vipaji vipya vinaendelea kuinuliwa na nawaahidi watanzania kusimamia haki. Ninachokiomba kutoka kwa watanzania ni kujiamini na kuonesha vipaji vyao kwani ukweli ni kwamba vipaji tunavyo na tunaweza.” Alisema Zahiri Zorro.

Katika mkutano huo na wanahabari miongoni mwa washiriki wa Tusker Project Fame miaka ya nyuma alikuwepo, Aneth Kushaba. Alisisitiza suala la kujiamini kama nguzo ya mafanikio katika kuhakikisha mshiriki anarudi na ushindi. Tafadhali kunywa kistaarabu. Haiuzwi kwa walio chini ya umri wa miaka 18