Joachim Mushi, Same
MGOMBEA mwenza nafasi ya uraisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu ameanza rasmi kampeni za kuomba ridhaa ya chama chake kupewa ridhaa na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro ya kuongoza tena nchi.
Samia ameanza ziara rasmi katika Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Same na kufanya mikutano ya hadhara katika Kata ya Hedari na baadaye wilayani Mwanga. Bi. Samia alilazimika kutembelea kituo cha Afya cha Hedaru na kuwasalimia wagonjwa na akinamama waliokuwa wakihudumiwa katika kituo hicho.
Akihutubia katika mkutano wa Hedaru alisema anajua kero ya maji katika vijiji vya eneo hilo na tayari Serikali ya CCM imeanza kuifanyia kazi na kabla ya 2016/7 watakuwa wamepata maji kutoka eneo la nyumba ya mungu.
Alisema ilani ya CCM imepanga kutoka shilingi milioni 50 kwa kila kijiji nchini hivyo kuwaomba wakichagu chama hicho. Alisema anatambua kero ya migogoro ya wafugaji na wakulima maeneo hayo hivyo wakipita yeye pamoja Mgombea Urais Dk. John Pombe Magufuli watahakikisha kero hiyobinamalizika kwa kupima ardhi ya eneo hilo ili kuonesha mipaka kuepuka migogoro.
Alisema kwa wakazi wa Jimbo la Same Mashariki anatambua kero ya barabara ya Mkomazi hivyo wakipata ridhaa watahakikisha kuwa barabara ya mkomazi inakamilika. Alisema ilani mpya ya CCM imepanga kujenga majosho na kutoa madawa ya mifugo kwa wafugaji ili nao waweze kunufaika na fursha kama ilivyo kwa wafugaji.
Samia katika msafara wake ameongozana na Amina Makilagi Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM, Anjela Kailuki Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania na Kamada wa Vijana wa Wilaya ya Same, Bi. Ummy Mwalimu Mjumbe wa Kamati ya kampeni ya Kitaifa na viongozi wengine wa Chama wa Wilaya na Mkoa wa Kilimanjaro.