MAMA Damali Kona mfanyabiashara katika Soko Kuu Mjini Musoma anaomba msaada kutoka kwa wasamaria ili kuweza kumsafirisha binti yake Bhoke Iddy kwenda kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mgonjwa huyo ameugua kwa muda mrefu na amekwisha pata matibababu kutoka katika hospitali ya Mkoa wa Mara na Bugando bila mafanikio na sasa amepewa rufaa ya kwenda Muhimbili.
Akizungumza na Shommi B Blog nyumbani kwake Mtaa wa Kenedy nyumba namba 77, mama Damali ameomba msaada kutoka kwa wasamalia wema na wenye muyo wa huruma ili aweze kujaribu kunusura maisha ya binti yake kwa madaktari bingwa.
Msomaji kuwa na moyo wa huruma na msaada wowote utapokelewa na wahusika ili kufanikisha matibabu ya binti huyu.
Unaweza kufikisha msaada wako moja kwa moja nyumbani mtaa wa kenedy nyumba namba 77 ama unaweza kuweka katika accaunti benki ya NMB A/C No 3031602562 au unaweza kuwasiliana na mama wa mgonjwa kwa simu hii 0754511991 au kumtumia kwa njia ya M-Pesa kwa namba iliyotajwa hapo juu. KUWA NA MOYO WA MSAADA LEO KWAKE KESHO KWAKO.
Taarifa na http://www.shommibinda.blogspot.com/