Haya ndio Magari Mawili aina ya ‘VOLKS WAGON AMAROK’ yaliyonunuliwa na Mfanyabiashara maarufu nchini Said Bhakresa.
Pichani Juu na chini ni Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD inayouza magari hayo Bw. Julius Guni (kushoto) akimkabidhi funguo pamoja na kitabu cha maelekezo ‘Manual Book’ cha magari hayo mwakilishi wa Bhakresa Bw. Omar Said kutoka Bhakresa Food Products.
Bw. Omar Said katika pozi baada ya kukabidhiwa rasmi magari hayo.
Bw. Omar Said akichomeka funguo kuwasha moja ya magari hayo.
Wow…..Kweli ni ‘VOLKS WAGON AMAROK’.
Volks Wagon ‘Amarok’ za Mzee Bhakresa.
Mkurugenzi mpya wa kampuni mpya ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Alfred Minja akiwajibika ofisini kwake kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na wateja wanapata taarifa za kutosha kuhusiana na kampuni hiyo pamoja na magari wanayouza.
Kanpuni hiyo imeanza kazi rasmi tarehe 1 Julai mwaka huu chini ya Mkurugenzi huyo mpya na tayari leo tarehe 11 Julai wamefanikiwa kuuza magari mawili aina ya ‘VOLKS WAGON AMAROK’.
Pichani Juu na Chini ni Fundi wa Kampuni ya Alliance Auto (T) LTD Bw. Dennis Dismas akifanya Services ya Magari ya Wateja wa Kampuni hiyo kwa Teknolojia ya kisasa inayotumia Kompyuta.