Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) limeandaa mashindano ya ngumi ya ubingwa wa Taifa 2012 yatakayofanyika kuanzia Septemba 17 hadi 22, 2012 ndani ya uwanja wa Taifa (indoor stadium). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga kwa vyombo vya habari leo amesema jumla ya mikoa 18 ya kimichezo itashiriki katika mashindano hayo.
Alisema lengo la mashindano hayo ni kupata timu ya taifa ya ngumi yenye sura ya kitaifa, itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania bara. Aliongeza kuwa ili kuanza maandalizi ya mapema na ya uhakika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola 2014, mashindano ya Afrika 2015, mashindano ya olimpiki 2016, ubingwa wa dunia na mashindano mbalimbali tutayopata mwaliko kwa ajili ya kuwakilisha taifa.
Aidha alisema awali mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kuanzia Septemba 15, 2012 lakini kutokana na uwanja wa ndani wa taifa kuwa na shughuri nyingine ya kimichezo ya ligi ya mpira wa kikapu, sasa mashindano hayo yataanza kutimua vumbi kuanzia Septemba 17, 2012.
“Hadi leo jumla ya mikoa kumi na nane (18) imethibitisha kuja kushiriki katika mashindano hayo, mikoa hiyo ni mikoa ya kimichezo ya Temeke, Kinondoni na Ilala. Mingine ni Ngome ya JWTZ, JKT, Magereza na Polisi. Mingine ni Pwani, Morogoro, Mbeya, Ruvuma, Dodoma, Kigoma, na Bukoba. mikoa mingine ni Tanga, Arusha , Tabora na Mwanza.”
Alisema uongozi wa BFT licha ya kutopata udhamini wa uhakika wa kufanikisha mashindano haya, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumejipanga vema kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha hali ya juu ili kufikia lengo la kupata timu ya taifa kwa wakati kwa maandalizi ya mapema.
Mashindano hayo yana takiwa kufanyika kwa bajeti ya milioni ishirini na sita (26,000,000/=).
Mabadiliko ya ratiba ya mashindano itakuwa kama ifuatavyo:-
TAREHE MUDA TUKIO
16/09/2012 Timu zote kuwasili dar es Salaam.
17/09/20123 1.00-4.00 Asb
4.00-5.00 Asb
5.00-7.00 Mch Kupima uzito na afya, uwanja wa taifa wa ndani.
Zoezi la draw na bye na ratiba ya mashindano.
Semina kwa waamuzi, timu manaja, makocha kwa ajili ya kupatiwa kanuni na sheria za mashindano.
18/09/2012 1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk Kupima uzito na afya, uwanja wa taifa wa ndani.
Gwaride la ufunguzi na kuanza mashindano hatua ya mtoano
19/09/2012 1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea hatua ya mtoano
20/09/2012 1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea kwa hatua ya robo fainali
21/09/2012 1.00-2.00 Asb
2.30-8.45Mch
9.00-2.00 Usk Kupima uzito
Mkutano mkuu wa BFT (indoor stadium)
Mashindano kuendelea hatua ya nusu fainali
22/09/2012 1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk Kupima uzito na afya.
Gwaride la kufunga na kuendelea kwa mashindano hatua ya fainali.
23/09/2012 Timu zote kuondoka
Aidha ajenda za mkutano mkuu wa wanachama wa bft ni mbili tuambazo ni kupitia na kupitisha rasmu ya katiba ya BFT na maandalizi ya uchaguzi wa BFT wa kuwapata viongozi makiniwa kuongoza BFT kwa kipindi cha miaka mine kuanzia marchi 2013 kwa mujibu wa katiba .