Yah: Uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT)
SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) kwa kulingana na Katiba yake, sheria na kanuni za Baraza la Michezo la Taifa (BMT)linatarajia kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa kuongoza Shirikisho kwa kipindi cha miaka mine ijayo.
Uchaguzi huo unatarajia kufanyika tarehe 07/07/2013 jijini Mwanza, sambamba na mashindano ya majiji. Nafasi zitakazogombewa ni kama ifuatavyo:-
1. Rais.
2. Makamu wa Rais.
3. Katibu Mkuu.
4. Mweka Hazina.
5. Wajumbe tisa wa kamati ya utendaji kwa nafasi zifuatazo:-
i. Kamati ya Mipango na Fedha
ii. Kamati ya Wamuzi na Majaji
iii. Kamati ya Mashindano na Vifaa
iv. Kamati ya Walimu, Ufundi na Utafiti.
v. Kamati ya Uhusiano, Habari na Masoko
vi. Kamati ya Wanawake.
vii. Kamati ya Maendeleo ya Mikoa na Taasisi za Umma.
viii. Kamati ya Tiba.
ix. kamati za Maendeleo ya Vijana na Wachezaji.
Fomu zitaanza kutolewa kesho tarehe 04/06/2013 katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
Usaili kwa wagombea wote utafanyika jijini Mwanza tarehe 05/07/2013
Ada ya fomu kwa wagombea zitatolewa kwa gharama zifuatavyo:-
• Kwa nafasi ya Rais ni Tsh. 150,000/=
• Kwa nafasi ya Makamo wa Rais, Katibu Mkuu na Mweka Hazina ni Tsh. 100,000/=
• Kwa nafasi za wajumbe wote tisa na Tsh. 50,000/=
Shirikisho linatoa wito kwa watanzania wenye uwezo wa kuongoza michezo kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi kama zilivyoelezwa hapo juu.
Taarifa hii inaletwa kwenu na
Makore Mashaga
Katibu Mkuu.