Waandamanaji watatu walijitokeza katika mkutano wa kumpinga nyota wa muziki Beyonce nje ya uwanja wa Mpira ya Marekani mjini New York.
Maandamano hayo yaliitishwa baada ya onyesho la msanii huyo wakati wa mapumziko ya mechi katika uwanja huo ambapo yeye na wacheza densi wake walivalia kama wanachama wa kundi la itikadi kali la Black Panthers.
Watu wengi nchini Marekani walisema kuwa onyesho hilo lilikuwa pigo kwa maafisa wa polisi pamoja na wale wanaoshinikiza sheria kufuatwa.
Lakini kulikuwa na waandamanaji wengi wa kumuunga mkono Beyonce katika maandamano hayo.
Onyesho hilo la Beyonce mapema mwezi huu lilishirikishi wacheza densi waliovalia kama wanachama wa kundi la Black Panther.
Kundi hilo lilikuwa la wapiganaji wa haki za weusi nchini Marekani kati ya mwaka 1960 na 1980.
Wakati mmoja kundi hilo la Beyonce lilitengeza umbo la X,ambalo wengi wanafikiri lilikuwa la kumuenzi mwanaharakati wa haki za kijamii nchini Marekani Malcom X ambaye alipigwa risasi mwaka 1965.