Wafanyakazi wa Benki ya Twiga Bancorp ambao wapo kwaajili ya kutoa huduma katika banda la Benki hiyo viwanbja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu Saba Saba wakilamba picha ya pamoja mbele ya Banda lao linalotoa huduma kamili za Kibenki huku wakiwa na tuzo ya Century International Gold Quality ERA waliyo ipata Genever kwa huduma bora .
Utoa huduma bora ndio nguzo na ngao ya Twiga Bancorp, pichani ni mteja akiwa na furaha wakati akizungumza na Afisa Mwandamizi Mwendeshaji wa Benki ya Twiga Bancorp Limited, Lydia Matembel, alipotembelea banda lao katika viwanja vya Maonesho Saba Saba.
Afisa wa Benki ya Twiga Bancorp Limited, Ernest Kikwasi, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo jana juu ya akaunti maalum ya watoto. Twiga Bancorp ni miongoni mwa benki zinazoshiriki katika Maonesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu JK Nyerere barabara ya Kilwa huku wakitoa huduma kamili za kibenki
Mmteja wa Twiga Bancorp akitoka kupata huduma katika banda la Benki hiyo kwa furaha baada ya kufanikiwa kutimiza alichotaka kwa wakati.