BENKI YA NMB YAFANIKISHA SIKU YA WAUGUZI MKOANI GEITA

Meneja Mahusiano Biashara za serikali Kanda ya Ziwa wa NMB Bi Suma Mwainunu Akitoa shukrani kwa wao kama Benki kushirikishwa kwenye shughuli hiyo ya siku ya wauguzi Duniani huku akihaidi kwa Kwa Benki yao kuendelea kushirikiana na serikali.

 

Mgeni Rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na mwakilishi wa makampuni ambayo yamefadhili shughuli ya siku ya wauguzi kutoka Benki ya NMB,Suma Mwainunu.

 

Maadhimisho ya Siku ya wauguzi Duniani yakieendelea.

 

Meneja Mahusiano Biashara za serikali Kanda ya Ziwa wa NMB Bi Suma Mwainunu Akitoa neno la Shukrani kwa wananchi pamoja na wauguzi ambao walikuwa wamekusanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mbongwe.

 

Meneja Mahusiano Biashara za serikali Kanda ya Ziwa wa NMB Bi Suma Mwainunu Akitoa shukrani kwa wao kama Benki kushirikishwa kwenye shughuli hiyo ya siku ya wauguzi Duniani huku akihaidi kwa Kwa Benki yao kuendelea kushirikiana na serikali.

Na Joel Maduka
BENKI ya NMB Tawi la Geita limetoa fulana 360 kwenye siku ya Wauguzi Duniani lengo likiwa ni kuendelea na Jitihada zake za kuwa karibu na jamii.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi ambapo Kimkoa yamefanyika mkoani Geita, Meneja Mahusiano Biashara za serikali Kanda ya Ziwa, Bi. Suma Mwainunu, amesema kuwa Benk hiyo inatambua thamani ya wauguzi na kwamba ndio maana wameamua kushiriki kwa kufadhili fulana hizo.

“Tumejisikia Vizuri sana na hivyo kwa niaba ya NMB tumeweza kushiriki hafla hii kwa kutoa Shilingi Milioni Tatu ambazo zimetumika Kununua Fulana ambazo mnaona wengi Tumezivaaa wauguzi hoyeeeeee,” Alisema Bi Mwainunu.

Hata hivyo, Bi. Suma Ameongezea kuwa Benki ya NMB ipo karibu na wateja na ndio maana wameshiriki hafla hiyo pamoja na wateja wao.

Aidha, Bi. Suma ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuiamini na kutumia Huduma ambazo zinatolewa na Benk hiyo yenye matawi mbalimbali nchi nzima na pia ametoa wito kwa uongozi wa Mkoa kushirikisha Benki ya NMB Katika maswala mbali mbali ya Kijamii nao wakiwa na uwezo wapo tayari kushirikiana nao.

Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa mgeni Rasmi, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ameishukuru Benki ya NMB kwa mchango wake katika kufanikisha sherehe hizo.