Benki ya Kiislam (PBZ) yaandaa futari

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akiwaongoza baadhi ya Viongozi wa dini na Serikali ‘kujisevia’ futari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na kufuturu pamoja na Makamu wa Rais Dk. Bilal na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa katika hafla hiyo, Agosti 8, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam baada ya hafla hiyo ya futari iliyoandaiwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Agosti 8, 2012 katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani-OMR