Bendi ya Mashujaa waandaa shindano maalum la mavazi ya kizamani

BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa Wanaposoposo’ Ijumaa ya
Juni 15 wameandaa shindano maalum la mavazi ya kizamani.

Wapenzi wa muziki wakaovaa mavazi ya kizamani watapata
zawadi shindano litakalofanyika kwenye ukumbi wa Business Park Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana meneja wa bendi hiyo Martin
Sospeter, alisema kuwa watu watakaoingia katikan onesho la bendi
hiyo watapata zawadi.

Alisema wamejipanga kuhakikisha wanatoa zawadi nzuri kwa
wapenzi watakakuja katika onesho hilo wakiwa na mavazi ya
kizamani, ili na vijana watambue kama nguo za zamani
zinaheshima na kutambulika.

Sospeter alisema kila atakayeingia akiwa amevaa vazi la kizamani
atakuwa amejiingia katika kushindania zawadi hizo ambazo ni
simu za mkononi na pesa taslim.

“Tumejipanga kuhakikisha tunarudisha mavazi ya kizamani ili
vijana watambue zamani kulikuwa na mavazi yake ambayo tufauti
na sasa na yalikuwa kivuti kikubwa kuliko sasa kila mtu anaamua
ajivalie kivvyake”alisema Sopeter.

Alisema bendi yao ya Mashujaa katika usiku huo pia itatuamia
nafasi hiyo kupiga nyimbo zao mpya ambazo bado hazijarekodiwa.
Sospeter alisema bendi hiyo chini ya Rais wake Charlz Baba ipo
vizuri, ikiwa inajiandaa kurekodi nyimbo zake mpya huku tayari
ikiwa imeshatoa nyimbo moja iiitwayo Risasi Kidole.