BASI la abiria aina ya Scania lenye namba za usajili T 591 ABK (Brazila) limepata ajali leo eneo la Mwida, Ubena kilomita kadhaa ukitokea Morogoro ambapo watu 10 wamepoteza maisha.
Akizungumzia ajali hiyo kutoka eneo la tukio Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Sarehe Mbaga amesema kati ya watu waliokufa wanawake ni 7 na wanaume watatu (3).
Kaimu Kamanda Mbaga amesema basi hilo aina ya Scania limepata ajali likiwa safarini kutoka Njombe kwenda Dar es Salaam na jumla ya abiria 19 wamejeruhiwa. Amesema uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na dereva haijajulikana kama naye ni miongoni mwa majeruhi au abiria waliokufa kwenye ajali.
Amesema majeruhi na maiti zimesafirisha kupelekwa hospitali ya Tumbi kwa msaada na miili kuhifadhiwa. Kati ya majeruhi wanawake ni nane na wanaume 11. Taarifa zaidi na tukio zima tutawaletea katika taarifa zetu mara baada ya kuzipata kwa kina.