WATU 12 wamefariki dunia baada ya treni ya abiria kuligonga basi lililokuwa likivuka reli jijini Nairobi, Kenya. Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema watu wengine waliokuwa kwenye basi hilo pia wamejeruhiwa kufuatia ajali hiyo mbaya.
Ajali za barabarani zinazosababisha idadi kubwa ya vifo hutokea kila mara nchini Kenya. Kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za barabara na mabasi yanayojaa abiria kupinduka, kila mara huendeshwa kwa mwendo wa kasi na kuyapita magari mengine ili kupata faida ya haraka.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, gari hilo lilikokotwa kwa takribani mita 500 kutoka eneo la ajali. Mkuu wa polisi jijini Nairobi Benson Kibui amesema basi hilo la abiria lilivuka reli wakati treni hilo lilipofika kwa mwendo wa kasi. Ajali hiyo ilitokea wakati wakazi wengi wa jiji walipokuwa wamejaa barabarani wakielekea sehemu zao za kazi majira ya asubuhi.
-DW