WATU 10 wanahofiwa kupoteza maisha huku 34 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Hood namba T.762 AVL aina ya Scania kuteketea kwa moto.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Joseph Lugila alisema ajali hiyo ilitokea katika Mbuga ya Mikumi baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso la lori lilobeba mafuta ya kupikia lililokuwa likitoka Morogoro kuelekea Iringa huku basi la Hood likitoka Mbeya kwenda Arusha.
Akifafanua zaidi juu ya ajali hiyo, Kaimu Kamanda Lugila alisema chanzo cha ajali hiyo ni kutanda kwa moshi uliyokuwa ukitokea pembeni mwa barabara baada ya uongozi wa Mikumi kuchoma nyasi kwa madai ya kusafisha mazingira. Alisema moshi ulikuwa umetanda kiasi cha kuwafanya madereva kushindwa kuona mbali barabarani.
Kamanda aliwataja majeruhi wa kuwa ni Benito Suga (34) kabila mhehe, mkazi wa Arusha, Peter Benilo (35) kabila Mhehe Kondakta wa basi hilo, mkazi wa Kibaha, Leila Mgina (23) kabila Mhehe, Amran Salehe (32) mkazi wa Iringa (Kabila Mhehe), Jemes Shitindi(36)mkazi wa Mbonzi na Mirika Maneno (7) mkazi wa Same.
Wengine ni Charles Yesaya (21) Mnyaturu mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni Mwanajeshi mwenye namba JWTZ-MT 0860, Jorada Mwasifike (46) mkazi wa Mbeya mkulima, Beatrice Mafuti(50) Mpare mkazi wa Ifunda, Joyce Kamkanila(11)mkazi wa Kihonda Morogoro, Asha Maneno(34) mkazi wa Same Moshi, Godson Sokreti (27) mkazi wa Arusha mwalimu wa Mrama Sekondari na Rose Zambi (43) myasa mkazi wa Mbeya mkulima.
Alitaja wengine ni Zenolina Marick (23) mkazi wa Arusha, Maria John (36) msambaa mkazi wa Iringa, Naropili Siroia (29) mmasai Arusha, Bahati Chonya (35) mwanasheria wa Manispaa ya Moshi, Salehe Tembo (42) mkazi wa Dar es Salaam dereva wa basi la Hood, Mbeleselo Joseph (33) daktari wa hospitali ya KCMC Moshi, Pius Mupitia (23) mfipa wakala wa Voda, Nestor Ngao (24) mkazi wa Mbeya ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha Dakawa.
Aliwataja wengine ni pamoja na Evans Mwasifiga (55) mnyakyusa mwalimu wa Sangu Sekondari, Godlivin Fred (23) mchaga mwanafunzi wa chuo cha Ruha, Monica Toloiya (59) mmsasi mkazi wa Loliondo Arusha, Richard Lubulu (52) mfanyakazi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Rukwa, Janny Stesioza(26) mfanyabiashara wa Moshi njia panda Himo, Teodori Raphael (20) mwanafunzi aliyehitimu seminari ya Same, Janny Fred (24) mwanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini Iringa na Erica Malimbwi(19) msambaa mwanafunzi wa sekondari ya JJ Muungano.
Majeruhi wangine waliotambulika ni pamoja na Cheso Lubulu (50) Mkinga, mkulima, Anastazia Kisera(48) mchaga mfanyabiashara na Kisa Mwakilubwa(40) Tukuyu Mbeya.