Barrick Yatoa Tuzo kwa Wafanyakazi Bora

Simon Shayo, mfanyanyazi wa Mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG) akiwa na tuzo ya ufanyakazi bora kwenye idara ya mahusiano ya jamii kwenye sherehe zilizofanyika mgodini hapo Machi 21, 2013. Shayo na timu nzima ya mgodi huo wamepewa tuzo hiyo kutokana na mradi wa kusaidia kikundi cha wanawake cha Nyabichune kijikwamue kiuchumi.

Lolence Kasekenya, mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (katikati) akiwa na zawadi yake ya mfanyakazi bora kwenye kitengo cha mahusiano ya jamii katika sherehe iliyofanyika kwenye mgodi huo tarehe 22 Machi 2013. Kulia ni Don Ritz, makamu wa rais mwandamizi wa kampuni ya Barrick anayeshughulikia usalama na uongozi na Kevin D’Souza, Mkurugenzi mwandamizi wa ABG upande wa mahusiano ya jamii na mazingira.

Marco Zolezzi, afisa mwandamizi (Chief Operating Officer) wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold, akitoa zawadi ya tuzo ya mfanyakazi bora kwa mfanyakazi wa kitengo cha uchunguzi cha mgodi wa Bulyanhulu, Gilbert Kalisa, kwenye sherehe zilizofanyika Machi 21, 2013, kwenye mgodi huo.

Igor Gonzales, makamu wa rais mtendaji na afisa mwandamizi (Executive Vice President & Chief Operating Officer) wa kampuni ya Barrick Gold Corp. (kushoto), akitoa zawadi ya tuzo ya mfanyakazi bora kwa Godfrey Nyabuzoki, mfanyakazi wa kitengo cha ulinzi cha mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold kwenye sherehe iliyofanyika Machi 21, 2013. Godfrey na wafanyakazi wengine watano wa kitengo cha ulinzi cha mgodi huo walionesha ujasiri mkubwa kukabiliana na kundi kubwa la wananchi waliovamia mgodi huo mwezi Machi mwaka huu na wafanyakazi hao wakaweza kumuokoa mwenzao aliyeumia. Kulia ni makamu wa rais wa kampuni ya Barrick Gold Corp. anayeshughulikia masuala ya ulinzi, Mark Wall.