Barmingham City ya Uingereza kuja Tanzania

Timu ya Barmingham City, kutoka nchini Uingereza

Kocha Msaidizi wa Timu ya Barmingham City, kutoka nchini Uingereza inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini humo, Andy Watson (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini leo kuhusu maandalizi ya ziara ya ujio wa timu hiyo nchini Tanzania mwezi Julai. Kocha huyo amefika nchini kwa ajili ya maandalizi na kukagua mazingira ya viwanja, Hoteli pamoja na miundombinu, ambavyo wameridhika navyo.Timu hiyo imeletwa na klabu ya Simba Sports kwa ajili ya mchezo wa kirafiki. Picha na mdau Mwanakombo Jumaa wa MAELEZO.