Baraza la Watoto Mkoani Mwanza Lataka Fursa Sawa kwa Watoto

Haleluya Benjamin ambaye ni Katibu wa baraza la Watoto mkoani Mwanza, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika hii leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha na kuwashirikisha watoto kutoka shule na taasisi mbalimbali.

Haleluya Benjamin ambaye ni Katibu wa baraza la Watoto mkoani Mwanza, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika hii leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha na kuwashirikisha watoto kutoka shule na taasisi mbalimbali.

 

Mwenyekiti wa Baraza la Watoto mkoani Mwanza, Paulina Mashauri, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika hii leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha na kuwashirikisha watoto kutoka shule na taasisi mbalimbali.
Wanafunzi wasichana wakiigiza michezo na maigizo mbalimbali
Wanafunzi wasichana wakiigiza michezo na maigizo mbalimbali
Kulikuwa na matukio mbalimbali ikiwemo wanafunzi kuonesha uwezo wao wa kujibu maswali
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akitoa ufafanuzi wa jambo
Na George Binagi, Mwanza
Baraza la Watoto mkoani Mwanza limeitaka jamii kutoa fursa sawa ya malezi bora kwa watoto
wa kike kama ilivyo kwa watoto wa kiume katika masuala mbalimbali ikiwemo fursa
ya kupata elimu.
Mwenyekiti wa baraza hilo, Paulina Mashauri, ameyasema hayo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike
Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika katika Uwanja wa Furahisha na
kuwashirikisha watoto kutoka shule na taasisi mbalimbali.
Naye Haleluya Benjamin ambaye ni Katibu wa baraza hilo amesema
bado watoto wa kike wanakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa fursa
ya kupata elimu, mimba na ndoa za utotoni hivyo ni vyema
jamii ikaungana pamoja katika kutokomeza changamoto hizo.
Msimamizi wa Watoto Baraza la Watoto mkoani Mwanza, Karus Masinde, ameiomba
jamii na serikali kwa ujumla kutoa kipaumbele kwa watoto wa kike katika masuala
mbalimbali ikiwemo ya kupata elimu pamoja na fursa za kiuongozi.
Kitaifa
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani yamefanyika mkoani Shinyanga yakiambatana
na kauli mbiu isemayo, Msichana Kushika hatam, ikiwa na lengo la kuihamasisha
jamii kutoa fursa kwa mtoto wa kike katika masuala mbalimbali katika jamii
ikiwemo kupata elimu na uongozi.