Baraza la Madiwani Kinondoni Lavunjwa Rasmi, Mwinyi Ashiriki

Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni, Yusuph Mwenda akimkabidhi jezi ya timu ya soka ya Kinondoni Municipal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi kama ishara ya kuwa mlezi wa timu hiyo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni, Yusuph Mwenda akimkabidhi jezi ya timu ya soka ya Kinondoni Municipal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi kama ishara ya kuwa mlezi wa timu hiyo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza kabla ya kuvunjwa kwa Baraza la Manispaa hiyo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza kabla ya kuvunjwa kwa Baraza la Manispaa hiyo.

Na Mwandishi Wetu
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imevunja rasmi Baraza la Madiwani ambapo mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa ni Rais mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi. Shughuli hizo zilitanguliwa na kikao cha baraza kupokea taarifa ya utekelezaji ambapo baada ya hapo mgeni rasmi Rais Mstaafu Mwinyi aliwasili na kufuatiwa na tukio la kukagua mabanda maalum yaliyoandaliwa yakionesha shughuli za kila idara na kupata maelezo.
Baadaye mgeni rasmi alihudhuria kikao rasmi cha kulivunja rasmi baraza hilo, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Jiji alilipongeza baraza la Madiwani na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondonikwa kazi nzito waliyoifanya ambayo Tanzania nzima wanaikubali ikiwepo ukusanyaji mzuri wa mapato na kumalizia kuwa Manispaa hii ni mfano mzuri wa kuigwa na Mstahiki Meya ni Meya wamfano kwa Tanzania nzima.
Katika kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni alilishukuru Baraza la madiwani kwa ushirikiano wao katika kutekeleza shughuli za maendeleo kwa Manispaa hiyo.

Alisema ni mengi yaliyotekelezwa na mengine kutokana na muda bado hayakuweza kutekelezeka, lakini ameahidi kuyatimiza yale ambayo wameyabariki yafanyike likiwepo la kujengwa kwa mtambo wa kuchakata taka huko mabwepande ambapo tayari na mkataba umeshasainiwa wa kuanza kujengwa kwa mtambo huo kwa msaada wa Homburg city.

Mgeni rasmi alitoa medani na vyeti kwa madiwani na kwa baadhi ya watendaji akiwepo Mkurugenzi. Katika kuitambulisha timu ya KMC-FC ambayo ni timu ya Manispaa ya Kinondoni mgeni rasmi alikabidhiwa jezi ya timu hiyo yenye jina lake Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi , hali kadhalika madiwani pia walipewa jezi hizo kila mmoja zenye majina ya kila mmoja na mkurugenzi aliwaomba kuitangaza timu hiyo na kuisaidia kwa hali na mali.

Aidha akizungumza katika hafla hiyo Mstahiki Meya, Yusuphu Mwenda aliwashukuru wakazi wa kinondoni kwa ushirikano. Akizungumzia maendeleo Meya alisema kumekuwa na ushiriki mpana wa wananchi katika maendeleo na pia uboreshwaji wa fedha za matumizi ya umma kwa kujenga shule, barabara na hospitali mbalimbali.

Alizungumzia pia Hospitali ya Mabwepande ambayo itakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi, akiongelea upande wa mapato alisema pato limeongezeka sana kutoka bil.11 kutoka kipindi cha nyuma hadi kufikia bil.35 hivi sasa. Kuhusu suala la vibali vya ujenzi kwa sasa vimekuwa vikitolewa na kupunguza msongamano na nia ni kuhakikisha vibali vya ujenzi vinapatikana ndani ya wiki moja, kuhusu usafi.

Aliongeza kuwa manispaa imekuwa ikishinda mfululizo katika mashindano ya usafi yanayosimamiwa na wizara ya afya pamoja na hilo aliongelea pia mpango kabambe wa alioucha katika mchakato wa utunzaji wa coco beach ili kuiboresha na kubadilishwa sura yake licha ya hayo manispaa hii pia imekuwa ikipata tuzo ya kutunza mahesabu vizuri. Pia alimshukuru Naibu Meya Songoro Mnyonge kwa ushirikiano na ushauri mzuri ambao amekuwa akimpa na mkurugenzi kwa ubunifu na ushirikiano wake pamoja na watendaji wote kwa ujumla. Kaimu mkuu wa mkoa akiongea alipopewa nafasi alisema haihitaji hata maelezo kuelezea Manispaa ya Kinondoni kwani juhudi zao zinaonekana kwa macho.

Mgeni rasmi akiongea katika hafla hiyo aliwashukuru kwa heshima hiyo waliyompa kwani alikuwa ana hamu kubwa ya kuja kuonana na watendaji wa Manispaa hii, alisifia kazi nzuri ya kuboresha maendeleo katika Manispaa hii na kuongeza kuwa Kinondoni ina uwezo wa kuendesha mambo vizuri kwa kuja kwake katika hafla hii amefundishika haswa.